Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wasanii 11 wa Kizazi kipya
wanaoendesha Tamasha la Uzalendo Tanzania kabla yha klulizindua rasmi kwenye
uwanja wa amani Mjini Zanzibar.
Na Othman Khamis Ame, OMPR Zanzibar.
KUNDI la wasanii
kumi na moja wa kizazi kipya Ndani ya Tanzania leo limeuvamia uwanja wa
michezo Amani kufanya Tamasha la Pili la Uzalendo Tanzania la Mwaka 2015...
Tamasha hilo
lililoasisiwa Mwaka Jana Mjini Dodoma na Rais wa Jamuhuri ya Muungano w
Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete lina lengo la kueneza ujumbe wa kudumisha
amani na Umoja Miongoni mwa Watanzania wote.
Mamia ya Vijana na
wapenda burdani walionekana kumiminika katika uwanja huo wa amani kushuhudia
waimbaji maarufu wa Kikazi kipya wakifanya vitu vyao jambo ambalo liliwafanya
wengi wa mashuhuda hao kuwacha viti vyao na kuanza kuserebuka.
Balozi Seif Ali Iddi
alisema kwamba wasanii Nchini Tanzania wana dhamana kubwa katika kuhakikisha
Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu kupitia fani yao ya sanaa.
Akilizindua Tamasha la
Pili la Uzalendo Tanzania la Mwaka 2015 Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif alisema wasanii ndio kioo cha jamii kinachoweza kutumika
katika kufikisha ujumbe na hata masuala ya maendeleo ya Kijamii.
Alisema mchango wa
wasanii katika jukumu kubwa linalolikabili taifa ndani ya mwaka huu wa 2015
kwenye kura ya maoni sambamba na uchaguzi Mkuu wa Mwezi wa Oktoba ni muhimui sana.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar aliwaomba wasanii hao kuhakikisha kwamba suala la Amani linakuwa ndio dira itakayowapa mwanga wa kuendeleza shughuli zao za sanaa
popote pale Nchini Tanzania.
Alisema Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla ni kisiwa cha amani Duniani, Hivyo juhudi za pamoja kati ya
wasanii na wananchi zinahitajika ili kuona lulu hiyo ya amani Nchini Tanzania
inaendelea kudumu.
Mapema Mjumbe wa
Kamati ya Tamasha hilo Nd. Shaib Ibrahim Mohammed alisema kwamba hilo ni
tamasha la kwanza kufanyika hapa Zanzibar likiwa na ujumbe wa kuendelea
kusisitiza umuhimu wa kudumisha amani, Umoja na Upendo miongoni mwa Jamii hapa
Tanzania.
Akitoa shukrani mwa
niaba ya Kundi hilo Msanii Miki wa Pili alizishukuru na kuzipongeza Serikali
zote mbili Nchini Tanzania kwa kufahamu umuhimu na mchango wa Wasanii.
Miki alisema fani ya
sanaa ndani ya ardhi ya Tanzania ilikuwa ikitambuliwa kama kazi ya kihuni
katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Alisema Wabunge wa
Bunge Maalum la Katiba wana haki ya kupongezwa kwa kujenga historia ya kudumu
iliyoainisha umuhimu wa kutambiliwa kwa kazi za wasanii na kupelekea kuingizwa
ndani ya Katiba inayopendekezwa.
|
No comments:
Post a Comment