Na Miza Kona na Maryam
Kidiko-Maelezo Zanzibar.
SERIKALI ya Mapinduzi
ya Zanzibar imesema ina lengo la kuinua vipaji vya wasanii wa Zanzibar ili
kuhakikisha kuwa kazi zinazotokana na jasho lao zinakuwa sehemu ya ajira kwao
ili kuondosha usumbufu wanaoupata..
Hayo ameyasema Naibu wa
Waziri wa Habari wa Utamaduni Utalii na Michezo Bihindi Hamadi Khamis wakati akijibu suala la Mhe. Wanu Hafidh
Ameir Nafasi za Wanawake aliyetaka kujua
kwa namna gani studio ile imewasaidia wasanii wa Zenj fleva kuinua vipaji vyao
kama vile studio ya Tanzania Bara.
Amesema Wizara ya Habari,
Utamaduni Utalii na Michezo ilijenga studio ya Rahaleo kwa ajili ya
Wasanii waliopo Zanzibar wakiwemo Wasanii wa Maigizo, Zenj fleva na wasanii wa
Taarab kwa kuinua vipaji vyao ili kuona kwamba
wanafaidika na kuweza kupata ajira.
“Vifaa vya kurikodia vimefika wiki iliyopita
bado vipo uwanja wa ndege kwa hatua ya kuvitoa na mafundi kutoka nje ya nchi
watakuja mwisho wa mwezi huu kwa hatua ya kuvifunga na tunatarajia wakimaliza
tu studio itaakuwa tayari kufanya kazi ya kurikodi na wasanii wetu watafaidika
na kazi zao”, amefahamisha Naibu huyo.
Amefahamisha kuwa
serikali inaendelea kuwasaidia wasanii wote waliojisajili katika Baraza la
Sanaa kwa kuwapatia mafunzo ya kuendeleza sanaa zao kupitia warsha na semina
kwa lengo la kuwapatia ujuzi wa kazi zao katika tasnia yao hiyo.
Ameeleza kuwa serikali
kupitia Wizara yake ya Habari Utamaduni na Utalii na Michezo inaendelea
kuwaelimisha wasanii wake kusajili kazi zao katika Jumuiya ya Haki miliki
(COSOZA) kwa ajili ya kudhaminiwa haki zao za uzeeni.
PIa Wizara inawapatia wasanii hao taaluma za
kufanya kazi zao katika kuandika, kurikodi na kufanya mauzo kwa lengo la
kufaidika na sanaa yao hiyo.
Wakati huo huo Baraza
la Wawakilishi limepitisha Mswada wa Sheria ya Miradi ya Maridhiano Namba 1ya
1999 na Kutunga Sheria Mpya kwa ajili ya Kuanzishwa na Kuendesha Mashirikiano
baina ya Sekta ya Umma na Binafsi na Mambo Mengine yanayohusiana na Hayo.
No comments:
Post a Comment