Na
Mwandishi Wetu,Zanzibar.
Tamko
hilo limetolewa jana na Naibu
Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka katika mkutano wake na
waandishi wa habari uliofanyika Afisi za UVCCM huko Gymkhana mjini Unguja.
Shaka
alisema CUF hakitashinda kwasababu hakina mgombea bora , kikiungwa mkono na wanasiasa wasioheshimika cha kizalendo na
hakiaminiwi kitaifa na kimataifa.
‘Kitendo
cha kutumia mgombea mmoja kila
mwaka ,kuongozwa na wanasiasa wenye
sifa za ubadhirifu wa mali za umma ,
kimeshindwa maperma kifute ndoto ya kuingia ikulu ”Alisema Shaka.
Aidha
alisema kitendo cha wafuasi wake kushangilia mitaani kifo cha Mwakilishi wa CCM jimbo la Magomeni Salmin
Awadhi Salmin ; kimekikosesha hadhi na kuthibitisha si cha kiungwana
kisichoweza kujenga umoja
wa kitaifa ila kitaleta mgawanyiko kati ya Pemba na Unguja.
Hata
hiyo Naibu huyo Katibu Mkuu wa UVCCM; ameitaka SMZ kuwasilisha mswada wa sheria
Baraza la Wawakilishi ili kuwa na chombo cha udhibiti na usimamizi wa mwenendo wa mitandao ya kijamii na tovuti.
“Mitandano
ya kijamii na tovuti kuendeshwa kinyume na maadili inahuzunisha , mitandao hiyo
inaweza kuchochea moto ambao ukiwaka na kusambaa hautopata mzimaji”Alisema Shaka .
Alisema
sehemu ya mitandao ya kijamii Zanzibar ina dhamira mbaya kwa nchi na Mapinduzi ya Zanzibar kwani
hutumika kukashifu watu, kufanya uchochezi , kejeli, mzaha na kedi kwa kushangilia kufa kwa watu.
“Tulidhani
vitimbi vya CUF kupiga na
kucheza ngoma wakila na kunywa kwa kufurahia kifo vingeishia mitaani ; cha kushangaza
wameviendeleza hadi kwenye mitandano
ya kijamii na tovuti”Alisema Shaka.
Shaka
alisema tukio la kushangilia kufa Mwakilishji wa CCM kimewakumbusha
walivyofanya CUF mwaka 1995 huko
Pemba kutia vinyesi
kwenye visima vya maji ya kunywa na kwenda kinyume na thamani ya utu na
ubinadamu.
“Tumeshangazwa
CUF kusherehea kifo cha mtu ,
jambo hili halijawahi kufanyika Tanzania; watanzania hawana mila na utamaduni wa kipuuzi tumeuona kutoka
kwao, bila shaka yapo mengi
ya kujiuliza”Alisema Shaka
Saka
alilaani kitendo hicho na
kusema hakitoi dhamira
njema ya kudumu Maridhiano
ya kisiasa yaliiofikiwa na kuundwa Serikali
ya umoja wa kitaifa na kqwamba
kinaweza kikawa
chanzo cha kusababisha mgawanyiko katika jamii .
Alisema UVCCM tayari wameshafanya mazungumzo na
Wawakilishi kutoka CCM , mmoja
miongoni mwao ameteuliwa awasilishe hoja binafsi Baraza la Wawakilishi kuitaka
Serikali ipeleke mswada wa sheria ya kudhibiti na kusimamia mwenendo wa mitando
ya kijamii na tovuti.
Pia
alisema Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kuinanga
Serikali anayoitumikia kwa kuiita ya kidhalimu ilhali ndiye Mshauri namba moja wa Rais wa Zanzibar
Dk. Ali Mohammed Shein, Shaka alisema kimeiogopesha UVCCM na hakikubaliki .
"Maalim
Seif ni kinara wa uzushi ; hali ya uchumi wa Zanzibar sio mbaya
kama alivyodai ; takwimu
zikionesha uchumi umekuwa
kwa asilimia 7.4 mwaka 2014
hadi 2015 ,kuna miundombinu ya barabara ya lami, vifo vya kinamama na watoto kupungua ;
kumalizika malaria na hakuna anaetembea umbali wa kilomita tano kufuata huduma za
afya"Alisema Naibu huyo Katibu Mkuu.
Alisema
hivi sasa hakluna mtu anayetembea zaidi ya kilimita tano kufuata shule na
kwamba Zanzibar imetimiza
malengo ya Milenia kabla
ya wakati uliowekwa na
Umoja wa Mataifa huku maendeleo ya kisekta yakiimarika
ambapo takriban vijiji
vyote Unguja na Pemba vina umeme wa uhakika na ikiwemo Pemba kuunganishwa katika gridi ya Taifa.
Vile
vile UVCCM imesema yakiorodhesha mafanikio ya kiuchumi na kijamii yaliofikiwa
chini ya SMZ mtu anweza kujaza vitabu na vitabu huku akiwataka
waandishi wa habari kumuuliza Maalim Seif ataje gharama anazotumia kwa ajili ya
kutibiwa kwake nchini India ambapo alisema kila safari huchota fedha za
umma shilingi milioni 8.
Kuhusu
Serikali ya Qatar kuitambua zaidi Zanzibar kuliko Tanzania, Shaka alisema
Seif ni muongo kwani akiwa
nje hupeperusha bendera ya Taifa ya Tanzaniana ; katika ramani ya Mataifa ya
Ulimwengu Zanzibar haimo, haipo katika Mataifa ya Afrika kama nchi Dola na madai ya Qatar kuijua
Zanzibar kuliko Tanzania ni madai ya kitoto.
No comments:
Post a Comment